Ukarimu

ukarasa wa maana wa Wikimedia

Ukarimu (kutoka neno la Kiarabu) ni tabia ya kutoa misaada na zawadi kwa watu wanaohitaji kweli.

Upande mmoja unashinda choyo, upande mwingine unashinda ubadhirifu, ambavyo vyote viwili ni vilema, kwa kuwa choyo kinanyima msaada unaowezekana kwa watu wanaouhitaji, wakati ubadhirifu unachezea mali kwa faida ya wasiohitaji zaidi.

Kama maadili mengine mengi, ukarimu unasimama katikati na juu ya vilema hivyo vinavyopingana.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukarimu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.