Sienna Tiggy Guillory (amezaliwa tar. 16 Machi 1975) ni mwigizaji wa filamu, tamthilia, na mwanamitindo wa Kiingereza. Mara nyingi alifanya kazi za uanamitindo mbali kidogo na sanaa ya uigizaji. Pia anafahamika zaidi kwa kuigiza kama Jill Valentine katika filamu ya Resident Evil: Apocalypse na kucheza tena kama Elf Arya Drottningu katika filamu ya Eragon.

Sienna Guillory
Sienna Guillory kwenye tuzo ya 2014 British Independent Film Awards
Sienna Guillory kwenye tuzo ya 2014 British Independent Film Awards
Jina la kuzaliwa Sienna Tiggy Guillory
Alizaliwa 16 Machi 1975 (1975-03-16) (umri 49)
Kazi yake Mwigizaji
Mwanamitindo
Miaka ya kazi 1996- hadi leo
Ndoa Enzo Cilenti (2002–hadi leo)

Huyu ni binti wa mzee Isaac Guillory, mpiga gitaa Mwiingereza-Mkuba. Guillory amepata kuigiza katika filamu nyingi za Kiingereza, na kisha baadaye filamu za Kiamerika. Si muda mrefu sana, amepata kucheza katika filamu za uzushi wa kisayansi na za kifantasia, ambazo zilitungwa kwa ajili ya vijana/watoto.

Maisha

hariri

Mahusiano

hariri

Guillory alianza kutembea na mwigizaji mwenzake Nick Moran kunako mwaka wa 1997. Wawili hao walikuja kuachana baada ya miaka mitatu, yaani kunako mwaka wa 2000. Mwaka huohuo baadaye, akaanza kutembea na Enzo Cilenti. Cilenti na Guillory walioana kunako mwaka wa 2002, na wakati sherehe za ndoa yao Guillory alivaa gauni ya harusi la bibi yake.[1][2] Wawili hao wanaishi mjini Los Angeles na London, lakini kunako mwaka wa 2007, wanandoa hao wakaamua kuweka makazi yao rasmi mjini Los Angeles.[3]

Filamu alizocheza

hariri

Filamu za kawaida

hariri
Mwaka Filamu Jina alilotumia Maelezo
1996 The Future Lasts a Long Time Blue
1999 The Rules of Engagement Denise
Star! Star! Lu
2000 Sorted Sunny
Two Days, Nine Lives Kate
The 3 Kings Roxana
Kiss Kiss (Bang Bang) Kat
2001 Oblivious Jessica
Late Night Shopping Susie
The Last Minute Kayak Girl
Superstition Julie
2002 The Time Machine Emma
2003 The Principles of Lust Juliette
Love, Actually Jamie's Girlfriend
Helen of Troy Helen
2004 Resident Evil: Apocalypse Jill Valentine
2005 In the Bathroom The Woman
Silence Becomes You Grace
2006 Rabbit Fever Newscaster
Eragon Arya Dröttningu
2007 El Corazón de la tierra Katherine English title:
The Heart of the Earth
Victims Completed
2009 Inkheart Resa Post-production

Televisheni

hariri
Mwaka Filamu Jina alilotumia Maelezo
1993 Riders Fenella Maxwell TV series
1995 The Buccaneers Lady Felicia Mfululizo mdogo wa katika TV
1999 Out of Sight Ingrid 2 sehemu
Dzvirpaso M 4 sehemu
2000 Take a Girl Like You Jenny Bunn TV movie
2003 Helen of Troy Helen Mfululizo mdogo wa katika TV
2004 Beauty Cathy Wardle Filamu ya TV
2005 Marple: A Murder Is Announced Julia Simmons 1 sehemu
The Virgin Queen Lettice Knollys Mfululizo mdogo wa katika TV
est. 2008 The Oaks Jessica Mfululizo wa katika TV
2008 Virtuality Rika Goddard Mfululizo wa katika TV

Marejeo

hariri
  1. Asome, Carolyn. "something deeply unfeminist about a miniskirt", Cinemania, 2004-05-27. Retrieved on 2007-09-30. Archived from the original on 2011-06-15. 
  2. "My hols: Sienna Guillory", travel.timesonline.co.uk, 2006-12-24. Retrieved on 2007-09-30. Archived from the original on 2023-03-23. 
  3. "LA Confidential", Company Magazine, Julai 2007, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-08-09, iliwekwa mnamo 2008-09-18 {{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date and year (link)

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons