Plutoni ni elementi katika mfumo radidia yenye alama Pu. Namba atomia ni 94 na uzani atomia ni 244. Jina limechaguliwa kutokana na sayari kibete Pluto.

Plutoni (plutonium)
kipande duara cha plutoni
kipande duara cha plutoni
Jina la Elementi Plutoni (plutonium)
Alama Pu
Namba atomia 94
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 244
Valensi 2, 8, 18, 32, 24, 8, 2
Densiti 19.816  g·cm³
Kiwango cha kuyeyuka 912.5 K (639.4 °C) 912,5 K ( °C)
Kiwango cha kuchemka 3505 K (3228 °C) K ​(3228 °C,
Asilimia za ganda la dunia 2 · 10-16 %
Hali maada mango
Mengineyo nururifu sana

Plutoni ni metali nururifu. Kiasili inatokea katika viwango vidogo sana penye madini ya urani kutokana na mbunguo nyuklia wa elementi hiyo ambao unaweza kuzalisha elementi nyingine. Vile viwango vidogo haviwezi kukaa mud mrefu kutokana na nusumaisha fupi ya plutoni inayozalishwa humo. Sehemu kubwa iliyopo leo hii imezalishwa katika matanuri ya nyuklia kutokana na urani.

Matumizi yake ni katika matanuri ya nyuklia na katika silaha za nyuklia. Matumizi yake ya kijeshi yalitangulia matumizi mengine: bomu lililobomoa mji wa Nagasaki nchini Japan katika Agosti 1945 na kusababisha vifo 60,000 lilitengenezwa kwa plutoni.

Umuhimu wa kiuchumi

hariri

Inatokea mara kwa mara kwa kuchoma urani katika tanuri nyuklia. Hivyo inasafishwa na kurudishwa kama fueli katika aina tofauti za matanuri ya nyuklia.

Matatizo yake ni kwamba unururifu wake ni mkali na hivyo kuna hatari ya kuishughulikia katika matumizi. Viwango vidogo sana vya plutoni vinaweza kusababisha kansa kama elementi hii inaingia mwilini kama vumbi au katika chakula. Baada ya kuzalishwa Plutoni inaendelea kuwa nururifu kwa muda mrefu na hivyo takataka ya kinyuklia yenye plutoni inahitaji kutunzwa mbali na watu kwa vipindi wa miaka elfu hata makumi elfu kadhaa.

Matumizi ya pekee ya plutoni ni katika beteri kwa ajili ya vyombo vya angani hasa vile vinavyokwenda mbali na jua na hivyo haviwezi kutumia nishati ya jua.

  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Plutoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Plutoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.