Lanthani
Lanthani ni elementi ya kikemia yenye alama ya La. Namba atomia ni 57. Ni sehemu ya kundi la elementi za Lanthanidi ikihesabiwa kati ya ardhi adimu. Rangi yake ni kidhahabu - nyeupe, lakini hewani inapata haraka ganda la oksidi lenye rangi ya kijivu. Ni laini na inaweza kukatwa kwa kisu.
Lanthani (Lanthanum) | |
---|---|
Jina la Elementi | Lanthani (Lanthanum) |
Alama | La |
Namba atomia | 57 |
Uzani atomia | 138.905 |
Valensi | 2, 8, 18, 18, 9, 2 |
Densiti | 6.126 g/cm3 |
Ugumu (Mohs) | 2.5 |
Kiwango cha kuyeyuka | 1193 K (920 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 3737 K (3464 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 17 ppm |
Hali maada | mango |
Jina linatokana na Kigiriki λανθάνειν lanthanein (kuficha) kwa sababu wanakemia walioitambua katika karne ya 19 waliona ugumu kuitenganisha na madini mengine.
Kuna matumizi ya lanthani katika teknolojia mbalimbali:
- "jiwe la kiberiti" huwa na asilimia 25-45 za lanthani
- wakala nakisishi (kiungo cha kuondosha oksijeni) katika uzalishaji wa aloi za metali
- inaungwa katika chuma ili kuongeza ufulikivu uzi
- oksidi ya lanthani huungwa katika kioo cha lenzi za kamera
- lanthani hutumiwa katika beteri za magari ya umeme aina ya NiMH; [1]
Marejeo
hariri- ↑ As hybrid cars gobble rare metals, shortage looms, tovuti ya Reuters, August 31, 2009
Viungo vya nje
hariri- The Industrial Chemistry of the Lanthanons, Yttrium, Thorium and Uranium, by R. J. Callow, Pergamon Press, 1967
- Extractive Metallurgy of Rare Earths, by C. K. Gupta and N. Krishnamurthy, CRC Press, 2005
- Nouveau Traite de Chimie Minerale, Vol. VII. Scandium, Yttrium, Elements des Terres Rares, Actinium, P. Pascal, Editor, Masson & Cie, 1959
- Chemistry of the Lanthanons, by R. C. Vickery, Butterworths 1953
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lanthani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |