Gali
Gali ni elementi. Namba atomia yake ni 31 kwenye mfumo radidia na uzani atomia ni 69.723.
Gali (Gallium) | |
---|---|
Fuwele za Gali tupu
| |
Jina la Elementi | Gali (Gallium) |
Alama | Ga |
Namba atomia | 31 |
Mfululizo safu | Metali |
Uzani atomia | 69.723 |
Valensi | 2, 8, 18, 3 |
Densiti | 5.91 g/cm³ |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 302.9146 K (29.7646 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 2477 K (2204°C) |
Asilimia za ganda la dunia | 1 · 10-3 % |
Hali maada | mango |
Ni metali haba na laini yenye rangi ya kifedha-buluu. Kwa halijoto ya duni ni mango kechu lakini huyeyuka tayari ikifikia kiwango cha 29 °C hivyo itayeyuka mkononi.
Hupatikana katika mitapo za boksiti na zinki.
Kampaundi zake hutumiwa kama nusupitisho katika teknolojia ya diodi.
Jina limetolewa na mwanakemia Mfaransa Paul Emile Lecoq de Boisbaudran aliyefumbua elementi hii mara ya kwanza mwaka 1875. "Gallium" larejea jina la "Gallia" ambalo ni jina la Kilatini la Ufaransa. Wengine huona ya kwamba alitaka kuweka kumbukumbu ya jina lake yeye mwenyewe kwa sababu "Lecoq" lamaanisha "jogoo" ambayo kwa Kilatini ni "gallus".
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |