Fahrenheit (kikamilifu vizio vya fahrenheit) ni kipimo cha halijoto. Alama yake ni °F.

Thermomita inayoonyesha vizio vya Fahrenheit na Selsiasi wakati moja
     Nchi ambako bado wanatumia Fahrenheit.      Nchi zinazotumia Fahrenheit pamoja na Celsius.      Nchi zinazotumia Celsius.

Skeli ya fahrenheit ilibuniwa 1724 na mwanafizikia Mjerumani Daniel Gabriel Fahrenheit. Ilikuwa skeli ya kupima halijoto iliyotumiwa sana duniani lakini wakati wa karne ya 20 skeli ya selsiasi ilichukua nafasi yake kwa sababu inalingana na vipimo sanifu vya kimataifa. Leo hii fahrenheit hutumiwa hasa Marekani na nchi chache nyingine kama Belize.

Kwenye skeli ya fahrenheit kiwango cha kuganda kwa maji ni 32 °F na kiwango cha kuchemka kwa maji ni 212 °F. Kwa hiyo kuna vizio 180 kati ya halijoto ya maji kuganda na kuchemka. Sifuri ya fahrenheit inalingana na −17,8 °C kwenye skeli ya selsiasi.

Mifano

hariri
  • Maji huganda kwa 32 °F na kuchemka kwa 212 °F.
  • Chumba kwa kawaida kinatakiwa kuwa na 70 °F.
  • Halijoto ya mwili wa kibinadamu uwa na 98.6 °F.
  • Sifuri halisi iko kwa –459.67 °F.

Tazama pia

hariri