Didake (yaani Mafundisho) ya Mitume Kumi na Wawili ni kimojawapo kati ya vitabu vya kale zaidi vya Ukristo, ambavyo viliandikwa na Mababu wa Kanisa na vinapatikana nje ya Biblia.

Kinakadiriwa kiliandikwa kati ya mwaka 70 na 150 BK katika mazingira ya Syria. Mwandishi wake hajulikani.

Kitabu kilipatikana tena mwaka 1873 huko Yerusalemu.

Lengo lake ni malezi ya Kikristo, yaani kupokeza mafundisho ya Mitume kwa katekesi juu ya maadili inayotofautisha "njia ya mauti" na "njia ya uzima", ikiwa na orodha ya vilema na maadili mema, ikifuatwa na matini ya liturujia na taratibu kuhusu ubatizo na ekaristi.

Sala iliyomo

hariri

Tunakushukuru, Baba yetu, kwa mzabibu mtakatifu wa Daudi mtumishi wako, uliotujulisha kwa njia ya Kristo Mwanao. Utukufu ni wako hata milele…

Kama vile mkate huu uliomegeka ulitawanyika vilimani, nao kisha kukusanywa umekuwa kitu kimoja, vivyo hivyo Kanisa lako likusanywe toka mipaka ya dunia katika ufalme wako: kwa kuwa utukufu na nguvu ni vyako kwa njia ya Yesu Kristo hata milele…

Tunakushukuru, Baba mtakatifu, kwa ajili ya jina lako takatifu, ulilolifanya likae mioyoni mwetu, na pia kwa ajili ya ujuzi, imani na uzima usio na mwisho ulivyotufunulia kwa njia ya Yesu Mwanao. Utukufu ni wako hata milele.

Wewe, Baba mwenyezi, uliviumba vyote kwa ajili ya jina lako, ukawajalia wanadamu chakula na kinywaji ili wakusifu; lakini sisi umetuneemesha chakula na kinywaji cha kiroh na cha uzima wa milele kwa njia ya Yesu Mwanao.

Kwanza tunakushukuru kwa kuwa u Mwenyezi. Utukufu ni wako hata milele.

Ulikumbuke, Bwana, Kanisa lako, uliokoe na kila uovu na kulikamilisha katika upendo wako, Ulitakase na kulikusanya toka pepo nne katika ufalme wako uliloliandalia; kwa kuwa nguvu na utukufu ni vyako milele.

Neema ya Mungu itufikie na ulimwengu huu upite. Hosana, Mwana wa Daudi! Aliye mtakatifu aje, na asiye hivyo aongoke. Maranatha! Amina!

  • Didakè yaani Mafundisho ya Mitume Kumi na Wawili na Waraka wa Mt. Klementi kwa Wakorinto, tafsiri ya B. Santopadre n.k. – ed. E.M.I. – Bologna (Italia) 1990 – ISBN 88-307-0321-4

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  • Audet, Jean-Paul, La Didache, Instructions des Apôtres, J. Gabalda & Co., 1958.
  • Draper, Jonathan, ed. 1996. The Didache in Modern Research (Leiden, New York and Cologne)
  • Holmes, Michael W., ed., The Apostolic Fathers: Greek Texts and English Translations, Baker Academic, 1 Desemba 1999. ISBN 978-0-8010-2225-8
  • Lightfoot, Joseph Barber, et al., Apostolic Fathers Archived 27 Septemba 2007 at the Wayback Machine., London: Macmillan and Co. 1889.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Didake kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.