Ali Larter
Alison Elizabeth "Ali" Larter (amezaliwa tar. 28 Februari 1976) ni mwigizaji wa fiamu na mwanamitindo wa zamani kutoka nchini Marekani. Ameanza kazi za uigizaji ni baada ya kuonekana kidogokidogo kwenye vipipindi kadhaa vya televisheni kunako miaka ya 1990. Kuanzia 2006 hadi 2010, Larter amecheza nyusika za Niki Sanders halafu ndugu wa kashinde wake-waliopoteana muda mrefu Tracy Strauss kwenye mfululizo wa TV wa ubunifu wa kisayansi wa kwenye NBC, Heroes.[2][3]
Ali Larter | |
---|---|
Larter at the 64th Annual Golden Globe Awards. | |
Amezaliwa | Alison Elizabeth Larter 28 Februari 1976 Cherry Hill, New Jersey, U.S. |
Jina lingine | Allegra Coleman[1] |
Kazi yake | Mwigizaji |
Miaka ya kazi | 1997–hadi sasa |
Ndoa | Hayes MacArthur (2009–hadi sasa) |
Larter ameanza kazi kama mwanamitindo lakini baada ya muda mfupi akajiingiza kwenye masuala ya uigizaji. Ameanza kujipatia umaarufu wa hali ya juu baada ya kushiriki kwenye filamu ya mwaka wa 1999, Varsity Blues. Hii ilifuatiwa na filamu ya kutisha ya House on Haunted Hill (1999), Final Destination (2000), na Legally Blonde (2001). Tangu hapo, akaanza kucheza kwenye nyusika za juu tena ikiwa ni pamoja na kurudia uhusika wake kwenye Final Destination 2 (2003), amecheza kama muhusika wa jina tu kwenye filamu ya Bollywood ya Marigold (2007) na kucheza kama muhusika wa mchezo wa video Claire Redfield kwenye Resident Evil: Extinction. Hivi karibuni, amecheza kwenye picha ya kusisimua ya mwaka wa 2009, Obsessed.
Larter amepewa jina kwenye orodha ya "Wanawake Wazuri Walio-Hai".[4] Ameolewa na bwana wake aliyedumu naye kwa muda wa miaka mitatu, Hayes MacArthur, kwa sherehe ndogo tu huko mjini Maine mnamo tar. 1 Agosti 2009.[5]
Maisha ya wali na Uanamitindo
haririLarter alizaliwa mjini Cherry Hill, New Jersey. Ana ndugu yake wa kike mkubwa aitwaye Kirsten, ambaye ni mwalimu. Yeye ni binti wa Bi. Margaret, mama wa nyumbani, na Danforth Larter, mkurugenzi wa usafiri w magari makubwa.[6][7] Alihitimu katika shule ya Carusi Middle School na Cherry Hill High School West. Larter ameanza kazi zake za uanamitindo akiwa na umri wa 14 wakati skauti wa uanamitindo amegundua kipaji chake mtaani kwao. Ameombwa kushiriki kwenye matangazo ya biashara ya Phillies na baadaye kutia saini mkataba wa kiuanamitindo na Ford Modeling Agency mjini New York. Larter baadaye karuka mwaka wake mkuu na kwenda kufanya uanamitindo nchini Japan na Australia. Akiwa na umri wa miaka 17, Larter akatulia kidogo nchini Japan.[8] Baadaye, mnamo 1995, kamsindikiza bwana'ke katika safari yake ya kuhamia mjini Los Angeles, California.
Filmografia
haririMwaka | Filamu | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
1999 | House on Haunted Hill | Sara Wolfe | |
Varsity Blues | Darcy Sears | ||
Drive Me Crazy | Dulcie | ||
Giving It Up | Amber | aka Casanova Falling | |
2000 | Final Destination | Clear Rivers | Young Hollywood Award for Breakthrough Performance Female Nominated — Blockbuster Entertainment Award — Favorite Actress - Horror |
2001 | American Outlaws | Zerelda 'Zee' Mimms | |
Jay and Silent Bob Strike Back | Chrissy | ||
Legally Blonde | Brooke Taylor Windham | ||
2003 | Final Destination 2 | Clear Rivers | |
2004 | Three Way | Isobel Delano | aka 3-Way Pia Mtayarishaji Msaidizi |
2005 | Confess | Olivia Averill | |
A Lot Like Love | Gina | ||
2007 | Marigold | Marigold Lexton | Bollywood |
Resident Evil: Extinction | Claire Redfield | ||
Homo Erectus | Fardart | aka National Lampoon's The Stoned Age | |
2008 | Crazy | Evelyn Garland | |
2009 | Obsessed | Lisa Sheridan | MTV Movie Award — Best Fight (amepeana na Beyoncé Knowles) Amechaguliwa — Teen Choice Award — Choice Movie Rumble (amepeana na Beyoncé Knowles) Amechaguliw — Golden Raspberry Award — Worst Supporting Actress |
2010 | Resident Evil: Afterlife | Claire Redfield | (inasubiri kutolewa) |
Televisheni
haririMwaka | Kipindi | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
1997 | Suddenly Susan | Maddie | Sehemu: "The Ways and Means" |
Chicago Sons | Angela | Sehemu: "Beauty and the Butt" | |
1998 | Chicago Hope | Samantha | Sehemu: "Memento Mori" |
Just Shoot Me! | Karey Burke | Sehemu: "College or Collagen" | |
Dawson's Creek | Kristy Livingstone | Sehemu: "The Dance" and "The Kiss" | |
2004 | Entourage | Ali Larter | Sehemu: "Pilot" |
2006–2010 | Heroes | Niki / Jessica Sanders / Tracy Strauss | Gracie Allen Awards — Outstanding Supporting Actress — Drama Series Teen Choice Award — Choice TV Actress: Action Adventure Nominated — Saturn Award for Best Supporting Actress on Television Nominated — Scream Award — Sexiest Superhero Nominated — SyFy Genre Awards — Best Supporting Actress/Television Nominated — Teen Choice Award — Choice TV Actress: Action Adventure |
Marejeo
hariri- ↑ "Biography for Ali Larter". IMBd. Iliwekwa mnamo 2010-06-27.
- ↑ "Heroes Cast Members, Tracy Strauss". NBC. Iliwekwa mnamo 2010-07-24.
- ↑ Feinburg, Daniel. "NBC's 'Heroes' Fascinates Larter", Zap2it, 2006-07-03. Retrieved on 2010-06-27. Archived from the original on 2012-09-26.
- ↑ "Ali Larter". Celebritywonder.com. Iliwekwa mnamo 2010-02-30.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help) - ↑ Everett, Christina. "'Heroes' star Ali Larter marries actor Hayes MacArthur in Maine", New York Daily, 2009-08-03. Retrieved on 2010-06-27. Archived from the original on 2009-09-07.
- ↑ "Ali Larter Biography". Tvguide.com. Iliwekwa mnamo 2007-08-27.
- ↑ Fahner, Molly. "Fun Fearless Female of the Year: Ali Larter", Cosmopolitan. Retrieved on 2010-06-27.
- ↑ "Ali Larter Biography". Yahoo.com. Iliwekwa mnamo 2007-08-27.
Soma zaidi
hariri- Wolf, Jeanne. Ali Larter, Always the Bad Girl. Parade Magazine. 24 Agosti 2009. Accessed 24 Julai 2010.
- Das, Lina. Actress Ali is a hero for our time. The Daily Mail. 9 Agosti 2007. Accessed 24 Julai 2010.
- Cavaco, Paul. Ali Larter: Her Allure Photo Shoot Archived 3 Februari 2010 at the Wayback Machine.. Allure. Accessed 24 Julai 2010.
- Our Heroine. Cosmopolitan. Accessed 24 Julai 2010.
- From Cherry Hill to Hollywood. The Philadelphia Inquirer. 15 Januari 2009. Accessed 24 Julai 2010.
- Hiltbrand, David. Split personalities make solid role for Ali Larter Archived 9 Mei 2012 at the Wayback Machine.. Chicago Tribune. 31 Januari 2007. Accessed 24 Julai 2010.
- Longsdorf, Amy.'Obsessed' star Ali Larter calls Allentown area a 'safe haven' Archived 22 Machi 2012 at the Wayback Machine.. The Morning Call. 26 Aprili 2009. Accessed 26 Julai 2010.
- Holding out for a hero. The Daily Mail. 1 Septemba,2007. Accessed 27 Julai 2010.
Viungo vya Nje
hariri- Ali Larter kwenye Internet Movie Database
- Ali Larter katika Yahoo! Movies
- Ali Larter katika All Movie Guide
- Ali Larter at People.com
- Ali Larter Archived 20 Julai 2010 at the Wayback Machine. at E! Online