Fedha
(Elekezwa kutoka Agenti (fedha))
Fedha kwa maana ya malipo au sarafu angalia makala ya pesa
Fedha (kutoka Kiarabu فضة fiddtan) ni elementi na metali yenye kifupi cha Ag (kutoka Kilatini: argentum) na namba atomia 47 katika mfumo radidia. Uzani atomia ni 107.86. Fedha huyeyuka kwa 1234.93 K (961.78°C) na kuchemka kwa 2435 K (2162°C).
Kiasili yatokea kama metali nyeupenyeupe na laini au kama mchanganyiko katika madini. Kati ya metali zote fedha ni wayaikaji na inapitisha vizuri umeme.
Fedha - Pesa
haririHuhesabiwa kati ya metali adimu na katika historia imetumiwa mara nyingi kama metali ya kutengenezea sarafu. Kwa sababu hiyo mara nyingi kwa Kiswahili neno "fedha" linatumiwa sawa na "pesa" au "sarafu".
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fedha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |