Teaching Documents by Sebastian Mbwillow
Utangulizi Dhana ya Sintaksia, ni taaluma ambayo huchunguza mpangilio wa maneno katika tungo na u... more Utangulizi Dhana ya Sintaksia, ni taaluma ambayo huchunguza mpangilio wa maneno katika tungo na uhusiano pamoja na vipashio vyake (viambajengo). Dhana ya sintaksia imefasiliwa na wataalamu mbalimbali, mathalani Richards (2010:579) sintaksia ni mfumo wa kanuni zitumikazo kupanga maneno yanayohusiana ili kuunda sentensi. Aidha TUKI (2014) inaeleza kuwa sintaksia ni tawi la isimu linalojishughulisha na miundo na uchanganuzi wa taratibu na kanuni za uhusiano baina ya maneno katika tungo. Katika fasili mbili za sintaksia tumeona jambo muhimu ambalo linazungumzwa katika taaluma ya sintaksia ni kuwapo kwa kanuni zinazotawala maneno yenye uhusiano katika sentensi za lugha husika. Katika kiwango hiki kuna kanuni zinazotumika kuweka maneno pamoja katika mpangilio mzuri unaokubalika katika jamii ya wazungumzaji wa lugha husika, ili kuleta uamilifu katika dhana nzima ya lugha. Hata hivyo, kanuni hizo huenda sambamba na kamwe hazifanyi kazi kwa kujitenga, yaani maneno lazima yawe na uhusiano. Hivyo basi, baadhi ya hizo kanuni hupatikana kupitia nyenzo kuu za sintsksia ambazo ni: ukategoria, ufuatano, kiimbo na viambishi. Nyenzo hizi zitaelezwa kwa katika sehemu inayofuata ya kazi hii. 01 Ukategoria Kategoria za kisintaksia ni vipengele vya lugha vinavyobainishwa kiumbo, kidhima na kimaana ili kutumika katika uchambuzi wa kisintaksia. Kategoria husaidia kuonesha mahusiano ya maneno katika sentensi kwa lengo la kuleta upatanisho wa maneno katika sentensi. Kategoria za kisintaksia zina viwango vikuu viwili ambavyo ni msamiati na kisarufi. Kategoria za kimsamiati, ni kategoria ambazo zina maudhui ya kimaana, kwa mujibu wa Rauh (2010:264-2) katika uanishaji wa kategoria, anaeleza kuwa katika lugha ulimwenguni kuna kategoria za msingi (primary categories) na akataja kuwa kategoria za msingi ni mbili tu,
Kazi hii inahusu nafasi ya mwanamke katika ngano za Kiswahili. Ngano ni mojawapo ya kipera cha ha... more Kazi hii inahusu nafasi ya mwanamke katika ngano za Kiswahili. Ngano ni mojawapo ya kipera cha hadithi katika utanzu wa fasihi simulizi, vipera vingine katika utanzu wa hadithi ni visasili, tarihi pamoja na visakale. Na istilahi ya mwanamke katika kazi hii tunaifafanua kuwa, ni mtu mwenye jinsi ya Kike. Katika kuifanya kazi hii zitafafanuliwa istilahi muhimu zilizobebwa na swali letu ambazo ni dhana ya ngano na ngano za Kiswahili kutokana na mitazamo ya wataalamu mbalimbali na kisha kutoa tafsiri hizo kulingana na mtazamo wa kazi hii. Baada ya hapo tutajadili nafasi ya mwanamke kupitia ngano za Kiswahili kwa kumwangalia jinsi alivyochorwa kuwakilishwa katika mitazamo mbalimbali ya kijamii. 02 Fasili ya dhana Mulokozi (1989) anaeleza kuwa ngano (hurafa, vigano) ni hadithi za kimapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na watu kuelezea au kuonya kuhusu maisha. Anaendelea kueleza kwamba utanzu huu unajumuisha fani kadhaa kwa mfano Istiara, Mbazi na Kisa. Akifafanua fasili hiyo Samwel (2015) anasema, ngano hutumia viumbe na vitu vingine visivyo na uhai kama wahusika, ndege na wadudu. Muhando na Basilidya (1976) wanaeleza kuwa ngano ni aina maalumu ya hadithi ipatikanayo katika fasihi asilia ya jamii yetu, fasihi ambayo ilitumiazaidi akili na ubongo wa binadamu kwa kuhifadhiwa kwake. Wanaendelea kueleza kuwa ngano nyingi aghalabu ni fupi na kutokana na ufupi huo, hizi si hadithi zinazozungumzia mambo kwa undani sana. Hadithi hizo huingia moja kwa moja katika kulitoa wazo kuu, na kila kipengele kijengacho ngano kama vile wahusika, vielelezo na mizungu mingineyo huelemea katika wazo hilo (Msokile 1992:8). Kutokana na fasili hii neno asilia linatudhihirishia kwamba chanzo cha ngano ni jamii husika. Kwa mfano katika jamii za Kiafrika ngano zitahusu jamii za Kiafrika
Utangulizi Katika kazi hii tutajadili dosari za mjifunzaji na usasanyuzi Dosari. Usasanyuzi dosar... more Utangulizi Katika kazi hii tutajadili dosari za mjifunzaji na usasanyuzi Dosari. Usasanyuzi dosari ni njia ya kupambanua na kufafanua Dosari za mjifunzaji lugha ya pili kwa ajili ya kujua chanzo chake. Ujifunzaji wa lugha ni sawa na ujifunzaji wa maarifa mengine kama vile, biashara, uashi, udereve na makanika, hivyo katika kujifunza hupitia michakato wa makosa. Wajifunzaji wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya kwanza hupitia katika michakato fulani ya kubahatisha katika ujifunzaji wa Kiswahili ambayo katika kazi hii tutaichunguzwa, itasasanyuliwa, itaainishwa, itaelezwa na kufanyiwa tathimini. Kwanza ifahamike wazi kuwa mjifunzaji lugha hufanya makosa katika vipengele vikuu viwili; (i) Ujuzi /utambuzi(comprehension) (ii) Utamkaji/uzalishaji (production) Makosa ya ujuzi/utambuzi ni makosa ambazo hutokana na mjifunzaji kutoelewa tungo. Kwa mfano: 1 (a) Amemuwezesha kula (b) Amemuwezesha kura Makosa ya kutoweza kutofautisha fonimu /l/ na /r/ katika matamshi kunasababisha kutoeleweka kwa mawasiliano kwa mjifunzaji lugha. Aidha Dosari katikautamkaji, ni Dosari ambazo zinatokana na matamshi. Yaani makossa ya matamshi kwa kukosa kufikiri. Katika sura hii tutajikita zaidi katika makosa ya utamkaji/uzalishaji (production), kwa mtu ajifunzaye Kiswahili kama lugha ya kwanza. Mjifunzaji wa lugha yoyote ile au ujifunzaji wa namna yoyote ile huwa na kasoro za namna fulani katika ujifunzaji wake. Kasoro ni sehemu ya upataji wa stadi yoyote, kufanya makosa ni mchakato wa ujifunzaji na uamiliaji wa maarifa. Bloom (1970)mjifunzaji wa lugha ya pili
Kwa muda mrefu kumekuwa na mkanganyiko kati ya dhana hizi tatu ambazo ni UAMBISHAJI, UAMBIKAJI NA... more Kwa muda mrefu kumekuwa na mkanganyiko kati ya dhana hizi tatu ambazo ni UAMBISHAJI, UAMBIKAJI NA UNYAMBULISHAJI. Makala hii inajaribu kugusia kama mada chokozi ya kutaka mjadala mkubwa uanze ama uendelee hadi hapo tutakapokuwa tumeridhika na utafiti na uchunguzi mkubwa juu ya dhana hizi kwa ujumla. Naomba wanagenzi wote hasa wabobezi wa lugha hii kutafiti na kuandika kwa kiwango cha juu kuhusu lugha yetu hii adhimu.
Katika kulijadili swali hili ni vema awali ya yote tukajadili kidogo dhana ya neno nomino. Dhana ... more Katika kulijadili swali hili ni vema awali ya yote tukajadili kidogo dhana ya neno nomino. Dhana hii imefasiliwa na wataalamu mbalimbali kwa kutumia vigezo mbalimbali. Ni wazi pia ikasemwa kuwa dhana hii baadhi ya wataalamu huita jina/majina, hivyo katika mazingira kama haya basi nomino na majina huwa ni visawe vyenye kurejelea dhana moja. Kihore na wenzake (2003) wanafasili nomino kuwa ni jina linalotaja kitu, kiumbe hai, dhana au tendo lolote liwalo. Tukiyachunguza kwa umakini maelezo haya tunaona kwamba, yanaashiria kuwa katika uamilifu wake, nomino hufanya kazi ya kukipambanua au kukibainisha kitajwa kwa madhumini ya kukitofautisha na vitajwa vingine. Kihore na wenzake (washatajwa) wanagawa makundi makuu ya nomino matatu. Ifahamike kuwa baadhi ya wachambuzi wa nomino huja na makundi au aina chache zaidi ya hizi au nyingi zaidi. Hali hii hutokana na mtazamo wa mchambuzi. Makundi kwa mujibu wa Kihore na wenzake ni kama yafuatayo; Nomino jumuishi au nomino za kawaida. Aina hii ya nomino huhusu vitu, dhana, viumbe n.k.ambavyo vinatajwa kwa jumlajumla. Mfano; a) wanyama b) chakula c) wanafunzi d) shule nomino mahususi au nomino za pekee. Haya ni majina yanayotaja vitu, dhana, na viumbe Fulani maalumu na kwa kutoa ubainishi ulio wa wazi zaidi kuliko ilivyo katika nomino za kawaida. Yaani majina hapa huwa na kiwango kikubwa cha ubainishi.Tuone mifano; a) maralia, pepopunda, UKIMWI Nomino kikundi au nomino za majina ya jamii. Hizi ni nomino zinazotaja makundi kadhaa ya viumbe, Kihore na wenzake (2003). Massamba (2009) naye nasema nomino kikundi (collective nouns) ni nomino zinazohusu majina yanayotaja jumuia yenye sifa za namna moja. Wanatoa mifano inayofanana kama ifuatavyo.
Papers by Sebastian Mbwillow
Utangulizi Maneno ya lugha asilia yoyote iwayo ya binadamu huwa na mpangilio ulio maalumu. Mpangi... more Utangulizi Maneno ya lugha asilia yoyote iwayo ya binadamu huwa na mpangilio ulio maalumu. Mpangilio huo maalumu hufuata sheria, kanuni na taratibu zinazoiongoza lugha hiyo. Maneno ya lugha ya Kiswahili nayo yana mpangilio maalumu ulofuata sheria, kanuni, na taratibu zinazoiongoza lugha hii. Japo kuna aina nyingi za maneno katika lugha ya Kiswahili, kama vile nomino, viwakilishi, vivumishi, vitenzi, vibainishi, na kadharika, makala hii itashughulikia ruwaza za kimofolojia za aina za maneno ya vitenzi, vivumishi, vibainishi, numerali/namba na vielezi. Muundo wa Vitenzi vya Kiswahili Massamba (2004) anafasili kitenzi kuwa ni kipashio kinachotoa taarifa kuhusu tendo lilofanyika, linalofanyika na au litakalofanyika. Kihore na wenzake (2003) wanadai kuwa kitenzi ni aina ya neno linalotoa taarifa juu ya tendo linalofanyika au litakalotendwa na kiumbe au kitu. Kwa mtazamo wa wataalamu hawa wanaona kuwa kitenzi kama aina ya neno shurti lioneshe au kubainisha tendo. Tendo hilo laweza kuwa ni la muda ulopita, uliopo ama muda ujao. Pia Kihore na wenzake wanasisitiza kuwa tendo hilo litendwe na kiumbe au kitu. Ingawa fasili zao ni nzuri lakinai kunachangamoto kidogo. Changamoto hizo zinahusu vitenzi visivyohusu matendo ama kutendwa. Hebu tupitie mifano hapa chini: 1.(a) baba ni mwizi. (b) mama alikuwa shambani. (c) hii si hali nzuri kwako. Katika mfano huu, maneno yaliyo katika hati ya mlazo hapo juu, katika Kiswahili na kwa hakika katika muktadha huu ni vitenzi. Lakini maneno haya hayaoneshi kitu au kiumbe kitendo jambo linalozungumzwa katika sentensi hizi. Kwa hiyo kwa mujibu wa fasili za wataalamu hawa itakuwa ni changamoto kuhusisha maneno haya katika fasili zao.
Drafts by Sebastian Mbwillow
IKISIRI Kazi hii inahusu ushairi wa Kiswahili hususan wasanii wanawake wa ushairi wa Kiswahili wa... more IKISIRI Kazi hii inahusu ushairi wa Kiswahili hususan wasanii wanawake wa ushairi wa Kiswahili wakati na baada ya ukoloni 1979. Awali ya yote, ufafanuzi wa istilahi mbalimbali muhimu zinazojitokeza katika kazi hii utafanyika. Istilahi hizo ni pamoja na dhana ya ushairi na waandishi wanawake. Hata hivyo, katika kuewalezea wasanii katika ushairi wa Kiswahili, tutaanza kwa kuwaelezea wale waliojitokeza wakati wa ukoloni kisha wale waliojitokeza baada ya ukoloni na mwishoni tutatoa hitimisho la jumla. 0.1 Usuli Wataalamu wengi wanakubaliana kuwa asili ya ushairi wa Kiswahili ni tungo simulizi, hasa ngoma na nyimbo zinazofungamana na ngoma (Chiraghdin 1971:7&10, Chiraghdin na wenzake 1975:62, Shariff, 1988:70) kabla ya karne ya 10 BK, Ushairi wa Kiswahili ulikuwa ukitungwa na kughaniwa kwa ghibu bila kuandikwa (Mulokozi, 1999). Majilio ya wageni walowezi, hasa kuanzia kama mwaka 1000 BK, yalileta mambo mawili yaliyokuwa na athari kubwa na kudumu katika maendeleo ya baadaye ya ushairi wa Kiswahili, mambo hayo ni dini ya Kiislamu na taaluma ya uandishi kwa hati ya Kiarabu. Baada ya ujio wa wamisionari hususani waingereza katika maendeleo ya ushairi walileta mambo makuu matatu ambayo yalikuwa na mchngo mkubwa katika maendeleo ya Ushairi wa Kiswahili nayo ni elimu ilitolewa kupitia kuanzisha kwa shule, walileta hati ya kirumi na taaluma ya uchapishaji wa vitabu. Hivyo kutokana na mambo hayo, kuliibuka waandishi mbalimbali wanawake na wanaume wa kazi za ushairi wakati na baada ya ukoloni. Katika kazi hii, tutajikita kuwaangalia waandishi wanawake katika sehemu ya kiini cha kazi hii. 2.0 Utangulizi na ufafanuzi wa Istilahi.
Utangulizi Katika kazi hii tutajadili dosari za mjifunzaji na usasanyuzi Dosari. Usasanyuzi dosar... more Utangulizi Katika kazi hii tutajadili dosari za mjifunzaji na usasanyuzi Dosari. Usasanyuzi dosari ni njia ya kupambanua na kufafanua Dosari za mjifunzaji lugha ya pili kwa ajili ya kujua chanzo chake. Ujifunzaji wa lugha ni sawa na ujifunzaji wa maarifa mengine kama vile, biashara, uashi, udereve na makanika, hivyo katika kujifunza hupitia michakato wa makosa. Wajifunzaji wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya kwanza hupitia katika michakato fulani ya kubahatisha katika ujifunzaji wa Kiswahili ambayo katika kazi hii tutaichunguzwa, itasasanyuliwa, itaainishwa, itaelezwa na kufanyiwa tathimini. Kwanza ifahamike wazi kuwa mjifunzaji lugha hufanya makosa katika vipengele vikuu viwili; (i) Ujuzi /utambuzi(comprehension) (ii) Utamkaji/uzalishaji (production) Makosa ya ujuzi/utambuzi ni makosa ambazo hutokana na mjifunzaji kutoelewa tungo. Kwa mfano: 1 (a) Amemuwezesha kula (b) Amemuwezesha kura Makosa ya kutoweza kutofautisha fonimu /l/ na /r/ katika matamshi kunasababisha kutoeleweka kwa mawasiliano kwa mjifunzaji lugha. Aidha Dosari katika utamkaji, ni Dosari ambazo zinatokana na matamshi. Yaani makossa ya matamshi kwa kukosa kufikiri. Katika sura hii tutajikita zaidi katika makosa ya utamkaji/uzalishaji (production), kwa mtu ajifunzaye Kiswahili kama lugha ya kwanza. Mjifunzaji wa lugha yoyote ile au ujifunzaji wa namna yoyote ile huwa na kasoro za namna fulani katika ujifunzaji wake. Kasoro ni sehemu ya upataji wa stadi yoyote, kufanya makosa ni mchakato wa ujifunzaji na uamiliaji wa maarifa. Bloom (1970) mjifunzaji wa lugha ya pili siye pekee afanyae makosa katika ujifunzaji lugha, hata watoto wanapojinza lugha hufanya makosa. Kwa mfano "sikuli ugali mimi' ambayo maana yake "sili ugali mimi". Halikadhalika hata wazawa
ii IKIRARI NA HAKIMILIKI Mimi, Shaibu Issa Champunga, ninathibitisha kuwa tasnifu hii ni kazi yan... more ii IKIRARI NA HAKIMILIKI Mimi, Shaibu Issa Champunga, ninathibitisha kuwa tasnifu hii ni kazi yangu halisi na haijawahi kuwasilishwa na wala haitawasilishwa katika chuo kikuu kingine kwa ajili ya kutunukiwa digrii kama hii au digrii nyingine yoyote ile.
Kazi hii imejadili ruwaza za kimofolojia za kitenzi cha Kiswahili, mjadala huu utaongozwa na nadh... more Kazi hii imejadili ruwaza za kimofolojia za kitenzi cha Kiswahili, mjadala huu utaongozwa na nadharia ya Mofolojia Leksika ambayo inazingatia kuwa mofimu kama kipashio cha msingi cha uchanganuzi wa kimofolojia. Katamba (1993:89) anaeleza kuwa jambo la msingi katika modeli hii ni mofimu kama msingi wa uchambuzi wa kimofolojia. Mofimu hizo zimepangwa kiutaratibu maalum kiviwango ili kuunda neno. Waasisi wa nadharia hii ni; Siegel (1974) na Allen (1978). Wafuasi wengine ni pamoja na Pesetsky (1979), Kiparsky (1982b), Mohanan (1982), Halle na Mohanan (1982) na Pulleybank (1986). Wataalamu hawa wanakubaliana kuwa Mofolojia ya Kileksika ni mtazamo unaolenga kuelezea uhusiano uliopo kati ya mofolojia na fonolojia kwa kuonyesha kuwa michakato ya kifonolojia na Mofolojia ni sehemu ya leksika na hupangwa kiviwango. Kwa kutumia kanuni ya Kufuta Mabano, ambayo inashadadia kuwa mofimu zinazopachikwa katika mzizi ili kuunda neno hupangwa kiviwango maalum, kwa kuonesha mipaka ya vipashio vinavyojengwa na kategoria husika. Katika makala hii tutajadili ruwaza za kitenzi cha Kiswahili kwa kutumia nadharia ya Mofolojia Leksika kupitia kanuni ya Kufuta Mabano, tumependelea kutumia kanuni hii ili tuoneshe bayana utaratibu wa kujenga vitenzi vya Kiswahili na kudhihirisha mipaka ya vipashio vya kitenzi. 2.0 Ufafanuzi wa Nadharia ya Mofolojia Leksika Nadharia ya Mofolojia Leksika ni nadharia zalishi na nyambulishi inayohusisha kiwango cha mofolojia kama kiwango mahsusi cha lugha, nadharia hii inasisitiza kuwa vipashio vinavyounda maneno hupangwa kwa kufuata kanuni maalalum. Nadharia Leksika huonesha uhusiano wa sheria zinazojenga maumbo ya kimofolojia, na sheria hizo zinadhibiti maumbo hayo. Baadhi ya wataalamu walioiunga mkono nadharia hii wamejitahidi kuzibainisha sheria hizo za kuunda
Nafasi ya Mwanamke katika ngano za Kiswahili Na Shaibu Issa Champunga (2019) Shuaybichamps12@gmai... more Nafasi ya Mwanamke katika ngano za Kiswahili Na Shaibu Issa Champunga (2019) [email protected] 0715055555/0624555500 01 UTANGULIZI Kazi hii inahusu nafasi ya mwanamke katika ngano za Kiswahili. Ngano ni mojawapo ya kipera cha hadithi katika utanzu wa fasihi simulizi, vipera vingine katika utanzu wa hadithi ni visasili, tarihi pamoja na visakale. Na istilahi ya mwanamke katika kazi hii tunaifafanua kuwa, ni mtu mwenye jinsi ya Kike. Katika kuifanya kazi hii zitafafanuliwa istilahi muhimu zilizobebwa na swali letu ambazo ni dhana ya ngano na ngano za Kiswahili kutokana na mitazamo ya wataalamu mbalimbali na kisha kutoa tafsiri hizo kulingana na mtazamo wa kazi hii. Baada ya hapo tutajadili nafasi ya mwanamke kupitia ngano za Kiswahili kwa kumwangalia jinsi alivyochorwa kuwakilishwa katika mitazamo mbalimbali ya kijamii. 02 Fasili ya dhana Mulokozi (1989) anaeleza kuwa ngano (hurafa, vigano) ni hadithi za kimapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na watu kuelezea au kuonya kuhusu maisha. Anaendelea kueleza kwamba utanzu huu unajumuisha fani kadhaa kwa mfano Istiara, Mbazi na Kisa. Akifafanua fasili hiyo Samwel (2015) anasema, ngano hutumia viumbe na vitu vingine visivyo na uhai kama wahusika, ndege na wadudu. Muhando na Basilidya (1976) wanaeleza kuwa ngano ni aina maalumu ya hadithi ipatikanayo katika fasihi asilia ya jamii yetu, fasihi ambayo ilitumiazaidi akili na ubongo wa binadamu kwa kuhifadhiwa kwake. Wanaendelea kueleza kuwa ngano nyingi aghalabu ni fupi na kutokana na ufupi huo, hizi si hadithi zinazozungumzia mambo kwa undani sana. Hadithi hizo huingia moja kwa moja katika kulitoa wazo kuu, na kila kipengele kijengacho ngano kama vile wahusika, vielelezo na mizungu mingineyo huelemea katika wazo hilo (Msokile 1992:8). Kutokana na fasili hii neno asilia linatudhihirishia kwamba chanzo cha ngano ni jamii husika. Kwa mfano katika jamii za Kiafrika ngano zitahusu jamii za Kiafrika zinazoonesha ujasiri, uvumilivu
Ikisiri Makala hii imechunguza viangami katika lugha ya Kiswahili kwa kueleza maana, aina, tofaut... more Ikisiri Makala hii imechunguza viangami katika lugha ya Kiswahili kwa kueleza maana, aina, tofauti iliyopo baina ya viangami na viambishi, na matumizi ya viangami katika lugha ya Kiswahili. Uchunguzi wa data utaongozwa na nadharia ya Mofolojia Msingi Mofimu, ambayo imeasisiwa na Stump (1991) nadharia hii huzingatia mofimu katika uchunguzi wa maneno. Msingi mkuu wa nadharia hii ni kwamba maneno huunndwa na mofimu ambazo zimepangwa katika mpangilio maalumu mithili ya mkufu. Kwa hiyo, kupitia makala itaelezea viangami kwa mkabala wa kimofolojia katika lugha ya Kiwsahili.
Kazi ya Darasani (Udsm) 01 UTANGULIZI Mwambatano ni moja ya njia za uundaji wa maneno katika lugh... more Kazi ya Darasani (Udsm) 01 UTANGULIZI Mwambatano ni moja ya njia za uundaji wa maneno katika lugha ya Kiswahili, Lugha nyingi ulimwenguni hujiundia maneno kwa njia ya mwambatano, maneno ambatani yanawakilisha majina ya watu, vitu na mahali katika lugha, maneno ambatani ni maneno ambayo hutokana na muunganiko wa maneno sahili mawili au zaidi ambayo yanaleta maana. Kwa mujibu wa McCarthy (2002:61) anaeleza mara nyingi maneno ambatani hujitokeza kwenye nomino, yaani maneno ya kategoria moja ama tofauti huwekwa pamoja na kupata neno moja ambatani ambalo mara nyingi neno linalopatikana huwa ni nomino, na hali hii inajitokeza katika lugha ya Kiswahili kuwa mbinu mbatani huzalisha nomino, Kwa mfano Zima + Moto, (T+N) tunapata nomino: Zimamoto. Na mara chache sana kupata kategoria nyingine ya maneno kama vile vitenzi, kwa mfano neno chapchap, hii ni aina ya mwambatano wa mdundo sauti nao husaidia uundaji wa maneno mapya. Wataalamu mbalimbali wamefasili dhana ya mwambatano, Massamba (2009:60) anafasili kuwa ni hali ya vipashio huru viwili au zaidi kukaa pamoja ili kuwakilisha dhana moja mpya. Hapa anakusudia vipashio huru ambavyo vinajitosheleza kimaana huunganisha na kuunnda neno jipya, kwa mfano: 1 (a) Njugu + Mawe Njugumawe (b) Piga + Mbizi Pigambizi (c) Mwana + Kwetu Mwanakwetu (d) Mcheza +Kwao Mchezakwao Katika mafano 1 (a) tunaona Njugu ni kipashio huru na Mawe ni kipashio huru kingine ambacho kimeunganishwa na kupata neno moja ambatani ambalo ni Njugumawe. Hali kadhalika Piga na Mbizi katika 1 (b) ni maneno huru yaliyounganisha na kupata neno ambatani. Pamoja na mifano mingine 1 (c)-(d) ni muunganiko wa vipashio huru viwili na kupata neno ambatani. Kwa mujibu wa Haspelmath (2010:137) anafasili dhana ya mwambatano kuwa ni leksimu changamani ambayo inatokana na muunganiko wa leksimu mbili au zaidi. Akazidi kufafanua
Mwambatano ni moja ya njia za uundaji wa maneno katika lugha ya Kiswahili, Lugha nyingi ulimwengu... more Mwambatano ni moja ya njia za uundaji wa maneno katika lugha ya Kiswahili, Lugha nyingi ulimwenguni hujiundia maneno kwa njia ya mwambatano,maneno ambatani yanawakilisha majina ya watu, vitu na mahali katika lugha, maneno ambatani ni maneno ambayo hutokana na muunganiko wa maneno sahili mawili au zaidi ambayo yanaleta maana. Kwa mujibu wa McCarthy (2002:61) anaeleza maranyingi maneno ambatani hujitokeza kwenye nomino, yaani maneno ya kategoria moja ama tofauti huwekwa pamoja na kupata neno moja ambatani ambalo maranyingi neno linalopatikana huwa ni nomino, na hali hii inajitokeza katika lugha ya Kiswahili kuwa mbinu mbatani huzalisha nomino, Kwa mfano Zima + Moto, (T+N) tunapata nomino: Zimamoto. Na mara chache sana kupata kategoria nyingine ya maneno kama vile vitenzi, kwa mfano neno chapchap, hii ni aina ya mwambatano wa mdundo sauti nao husaidia uundaji wa maneno mapya. Wataalamu mbalimbali wamefasili dhana ya mwambatano, Massamba (2009:60) anafasili kuwa ni hali ya vipashio huru viwili au zaidi kukaa pamoja ili kuwakilisha dhana moja mpya. Hapa anakusudia vipashio huru ambavyo vinajitosheleza kimaana huunganisha na kuunnda neno jipya, kwa mfano: 1 (a) Njugu + Mawe Njugumawe (b) Piga + Mbizi Pigambizi (c) Mwana + Kwetu Mwanakwetu (d) Mcheza +Kwao Mchezakwao Katika mafano 1 (a) tunaona Njugu ni kipashio huru na Mawe ni kipashio huru kingine ambacho kimeunganishwa na kupata neno moja ambatani ambalo ni Njugumawe. Hali kadhalika Piga na Mbizi katika 1 (b) ni maneno huru yaliyounganisha na kupata neno ambatani. Pamoja na mifano mingine 1 (c)-(d) ni muunganiko wa vipashio huru viwili na kupata neno ambatani. Kwa mujibu wa Haspelmath (2010:137) anafasili dhana ya mwambatano kuwa ni leksimu changamani ambayo inatokana na muunganiko wa leksimu mbili au zaidi. Akazidi kufafanua
Ikisiri Maendeleo ya tekinolojia katika ulimwengu wa sasa yamepelekea uwepo wa mabadiliko katika ... more Ikisiri Maendeleo ya tekinolojia katika ulimwengu wa sasa yamepelekea uwepo wa mabadiliko katika Nyanja mbalimbali, kama vile katika elimu, uchumi, siasa, na hata katika mawasiliano. Uvumbzi vitu kama simu, tarakirishi, vifaa mbali mbalimbali vya mawasiliano kama visikizi sikio (earphone) na visikizi kichwa (headphone), tablet, na mashinde za kuchuja sauti. Vyote hivi vimepelekea uwepo wa mabadiliko makubwa hasa katika uwanja wa mawasiliano na hususani hapa katika ugha huu wa ukalimani. Ukalimani sasa umerahisishwa na kujiongezea aina zake ama kujitanua. Matharani ukalimani nong'onezi ambao awali agharabu ulifanywa baina ya mkalimani na mteja mmoja au kwa nadra sana wawili, sasa ukalimani huu umepanuka na kuweza kuhudumia mamia ya watu kwa kutumia vifaa maalumu vya mawasiliano ambapo mkalimani huweza kukaa katika kizimba chake na wateja wake wakavaa vifaa maalumu vya kupokea sauti na wakafaidi ukalimani wake pasi na taabu yoyote (taz. Pöchhacker,2004:18). Makala haya yamelenga kuonesha faida za utumizi wa tekinolojia katika ukalimani.
Iksiri " Kwani tusi kitu cha ajabu? Wewe hujawahi kutukana? " Maneno haya yalisemwa na mwanamke m... more Iksiri " Kwani tusi kitu cha ajabu? Wewe hujawahi kutukana? " Maneno haya yalisemwa na mwanamke mmoja aliyekuwa akimpolomoshea matusi jirani yake, wakati watu wakijaribu kumzuia asiendelee kutukana. Yawezekana kuna watu wengi katika dunia ya leo huwashangaa baadhi ya watu wanaoona kuwa baadhi ya manenno ni matusi na hivyo hayafai kuongelewa mbele za watu. Pia bado kuna watu hadi leo ambao huwashangaa wale wanaochukulia kuwa matusi ni maneno ya kawaida na hivyo yaweza kutumika popote na yeyote. Yawezekana pia tukawa sote tunauelewa tofauti na mtazamo tofauti juu ya dhana na maana ya matusi. Matusi maana yake nini? Je tusi ni tusi wakati wote na kwa kila mtu? 1.0 Utangulizi Makala haya yanaangazia juu ya dhana nzima ya matusi. Lengo hasa la makala haya ni kutaka kujua kama matusi yaweza kuwa na maana chanya. Hii ni kutokana na mabadiliko ya watu katika miaka ya hivi karibuni kuzidi kutumia maneno ambayo huaminika kuwa ni matusi hadharani. Siku hizi imekuwa kawaida karibia kila mahali kusikika matusi. Iwe ofisini, iwe shuleni, sokoni, nyumbani na maeneo mengine mengi. Hali hii imepelekea baadhi ya watu kuwa na maswali mengi kuhusina na dhana hii ya matusi. Hivi matusi ni nini basi? Kwa nini watu hutukana? Inakuwaje mtu anazoea kutukana? Kwa nini wengine wakitukanwa wanakasirika na wengi hawakasiriki? Maswali haya na mengine mengi ambayo baadhi ya wanajamii wamekuwa wakijiuliza ndiyo yamepelekea makala haya kuja ili kujaribu kujibu maswali hayo. 2.0 Je Matusi ni Nini? Matusi au tusi ni neno chafu la kumuudhi mtu, Kamusi ya Kiswahili Sanifu(2013:569). Maana hii ya matusi inatueleza juu ya neno au maneno, ambayo agharabu lazimwa yasemwe. Ingawa kwa waswahili matusi yanaweza kufanywa pia. Kwa kuwa lengo la makala haya ni kuchunguza matusi hasa ya kusemwa, matusi ya aina nyingine yataachwa na pengine kutoa fursa kwa wengine kuyachunguza. Kwa hakika matusi ni maneno au ishara za kuudhi, kukera, kudharaulisha, kuvunja heshima na hata kuharibu sifa ya mtu. Matusi yaweza kutukanwa kwa kusemwa kama vile bwege, msenge na kadharika. Pia yaweza kutukanwa kwa ishara kama vile ya kumuoneshea mtu dole la katikati. Matusi katika mira za waafrika na hasa Watanzania huchukuliwa kuwa ni mwiko-jambo ambalo mtu hawezi kulitenda kwa sababu ya imani, mazoea au tabia. Tokea enzi na enzi wazazi walijitahidi kuwazuia watoto wao wasipate kutamka maneno ambayo iliaminiwa kuwa ni matusi. Hali hiyo ikawa tabia na ikatujengea imani ya kuwa baadhi ya maneno na ishara ama vitendo havifai ama kutendwa na kutamkwa mbele za watu au hata kutojaribu kusikia au kujihusisha navyo hasa katika
Ikisiri Kategoria za maneno katika lugha ya Kiswahili zimekuwa na mkanganyiko mkubwa hasa katika ... more Ikisiri Kategoria za maneno katika lugha ya Kiswahili zimekuwa na mkanganyiko mkubwa hasa katika idadi yake. Kila mtaalamu amekuwa na idadi tofauti na mtaalam mwingine, kwa mfano Khamis, (2011) ameainisha aina tisa za maneno sawa na Wesana-Chomi (2003); Thompson na Schleicher (2001) wanaainisha aina saba za maneno ya kiswahili. Pia kwa upande mwingine wataalamu hawa licha ya kutofautiana huko kwa idadi ya maneno, pia wanatofautiana kwa istilahi wanazozitumia. Kwa mfano Kihore na wenzake (2003) wanatumia istilahi Viingizi wakirejelea Vihisishi kama alivyotumia Wesana-Chomi (2003) na Thompson na Schleicher (2001). Hali kadhalka katika kiswahili kuna baadhi ya kategoria za maneno zimetafitiwa sana na nyingine hazijatafitiwa sana, kwa mafano, vitenzi na nomino vimetafitiwa kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na vihisishi, vihusishi na vibainishi. Makala haya yamelenga katika kuchunguza kwa kutumia mkabala kikazi na kifasili na kubaini aina ya maneno ambayo wataalamu wengi bado hawajaikubali. Hii ndio sababu ya kuteua mada hii katika makala haya ili kuweza kuonesha uwepo wa aina hii (kibainishi) ya neno katika lugha ya kiswahili.
Kazi hii imejadili ruwaza za kimofolojia za kitenzi cha Kiswahili, mjadala huu utaongozwa na nadh... more Kazi hii imejadili ruwaza za kimofolojia za kitenzi cha Kiswahili, mjadala huu utaongozwa na nadharia ya mofolojia Leksika ambayo inazingatia kuwa mofimu kama kipashio cha msingi cha uchanganuzi wa kimofolojia. Katamba (1993:89) anaeleza kuwa jambo la msingi katika modeli hii ni mofimu kama msingi wa uchambuzi wa kimofolojia. Mofimu hizo zimepangwa kingazi ili kuunda neno.Waasisi wa nadharia hii ni; Siegel (1974) na Allen (1978). Wafuasi wengine ni pamoja na Pesetsky (1979), Kiparsky (1982b), Mohanan (1982), Halle na Mohanan (1982) na Pulleybank (1986).Kwa kutumia kanuni ya kufuta mabano, ambayo inashadadia kuwa mofimu zinazopachikwa katika mzizi ili kuunda neno hupangwa kidarajia, kwa kuonesha mipaka ya vipashio vinavyojengwa na kategoria husika. Tutajadili ruwaza za kitenzi cha Kiswahili, tumependelea kutumia kanuni hii ili tuoneshe bayana utaratibu wa kujenga vitenzi vya Kiswahili na kudhihirisha mipaka ya vipashio vya kitenzi. 2.0 Ufafanuzi wa nadharia ya mofolojia Leksika Nadharia ya mofolojia Leksika ni nadharia zalishi na nyambulishi inayohusisha kiwango cha mofolojia kama kiwango mahsusi cha lugha, nadharia hii inasisitiza kuwa vipashio vinavyounda maneno vimepangwa kidarajia kimsonge ambapo vipashio vidogo huungana ili kuunda vipashio vikubwa zaidi (Kiparsky 1982). Nadharia Leksika huonesha uhusiano wa sheria zinazojenga maumbo ya kimofolojia, na sheria hizo zinadhibiti maumbo hayo. Baadhi ya wataalamu walioiunga mkono nadharia hii wamejitahidi kuzibainisha sheria hizo za kuunda maneno kimofolojia, kwa mfano: Katamba (1993:104) anafafanua sheria zinazounda maumbo ya kimofolojia ikiwa pamojana: (i) Mzizi/shina linaloathiriwa, (ii) viambishi vilivyojenga neno, (iii) upachikaji wa viambisha aidha mbele au nyuma ya mzizi
Uploads
Teaching Documents by Sebastian Mbwillow
Papers by Sebastian Mbwillow
Drafts by Sebastian Mbwillow